Upinzani unadai kuwa rais Nkurunziza anakiuka katiba ya taifa na mapatano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa mujibu wa Msemaji wa rais ,Gervais Abayeho uchaguzi huo umeahirishwa
kutoka tarehe 15 hadi tarehe 21 kufuatia shinikizo la viongozi wa kanda
ya Afrika mashariki na Kati.
Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya
Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta waliendekeza uchaguzi uahirishwe kufuatia mgogoro wa
kisiasanchini Burundi.
No comments:
Post a Comment